Posts

PASAKA NJEMA

Image
Bwana Atembee nanyi Wapendwa wasomaji wa Blog hii; Nawatakia pasaka njema iweni na Amani ya Kristo iwe Pamoja nanyi Daima

ASANTE MUNGU

Wewe ni Mwema sana kwangu

Children and Youth Ministry (CYM)

Image
The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) CHILDREN AND YOUTH MINISTRY (CYM) Jengo la Kanisa la FPCT-SEPUKA IDARA YA WATOTO NA VIJANA FPCT-SINGIDA Idara ya Watoto na vijana ya Misheni ya Singida wamefanya ziara nyingine tena katika kanisa la Fpct-Sepuka ambalo ni moja ya tawi katika Parishi ya Kaselya ambayo imo ndani ya misheni ya Singida na kufanya maombi katika kanisa hilo Pamboja na hayo; pia wamejionea mambo mbalimbali ambayo hayafurahishi katika kanisa hilo kulinganisha na wakati tulionao sasa. Moja ya mambo hayo ni pamoja na uchakavu wa majengo mfano Jengo la kuabudia (kanisa), Nyumba ya Utumishi katika kanisa hilo na maeneo mengine ikiwemo Vyoo n.k. Inasemekana Kanisa lilijengwa zamani kidogo na kufanyiwa ukarabati mdogo mwaka 2000 lakini baada ya hapo limeendelea kuchakaa. Mpaka sasa jengo hilo limebaki kuwa wazi baada ya Milango na madirisha yake kuibwa na ndicho kilicho fanyika hata kwa nyumba ya kanisa hilo ambayo pia haina milango wala madirisha kutokana ...

HONGERA FPCT-SINGIDA

Image
Dr. Paul Samwel baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari  Kwa mara ya kwanza mmoja wa Viongozi wa kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania ametunukiwa shada ya juu ya Udaktari; akiongea na waandishi waandishi wa habari Dr. Paul Samwel hakuacha kuongelea uchaguzi ujao na kusema kuwa anaamini kuwa uchaguzi huu utakuwa wa amani na pia viongozi ambao Mungu amekusudia kuiongoza Tanzania Watapatikana tu!

MO "SIGOMBEI TENA!!!

Image
Wakati Tanzania inakaribia kuingia katika duru ya Uchaguzi Mkuu  Bw. Mohamed Gulam Dewji ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo ambayo ameitumikia kwa muda wa miaka kumi sasa Jimboni mwake. Bw. Dewji ametangaza uamuzi huo jana tarehe 8/7/2015 mjini Singida wakati akiwasomea wananchi wa Jimbo lake taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005/2010 katika jimbo la Singida Mjini. Akiwahutubia maelfu ya wananchi ambao walikusanyika ili kuisiliza hotuba yake Dewji ameelaza mambo mbalimbali ambayo yamefanikiwa kufanyika katika kipindi chake cha Umbunge jimboni mwake, Dewiji ameeleza kuwa katika kipndi chake chote cha Ubunge  amefanikiwa kusimamia ujenzi wa Shule na kuongeza Vyumba vya Madarasa katika shule mbalimbali Jimboni mwake pamoja na hayo umo pia Ujenzi wa miradi ya Maji ambayo imekwisha kukamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa jimbo la Singida mjini. Miradi hiyo ni pamoja ule wa Irao na mradi wa maji kutoka Mwankoko ambayo yote kwa pamoja...

UWW-SINGIDA KUAZIMISHA SIKU YA MAMA DUNIANI

Image
       Wamama wakitoka katika moja ya wodi za wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa Katika kuazimisha siku ya wanawake ulimwenguni Umoja wa Wanawake Watumishi (UWW) wa kanisa la FREE PENTECOSTAL CHURCHES OF TANZANIA-(FPCT) Singida wameazimisha siku yao kwa kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na Mahabusu katika Gereza la Mkoa. Matembezi hayo ya wamama wa Kanisa yaliongozwa na Mwenyekiti wa UWW wa Kanisa hilo Mrs. Betheli (Mama Wawili) ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Watumishi (UWW) kanisa la Free Pentecostal Churches of Tanzania Jimbo la Singida. Pamoja na kufanya matembezi hayo,   Wamama hao wamewapatia pole kwa   kuwapa vitu mbalimbali kama vile sabuni,   mafuta ya kupaka pamoja na mavazi. Pia   Mwenyekiti huyo amesifu mapokezi ya   wahudumu katika maeneo hayo yote ambayo  walifanikiwa kutembelea. Wamama hao wamesema kuwa ni vema kuwakumbuka wenzao wenye shida mbalimbali hasa ...