MO "SIGOMBEI TENA!!!

Wakati Tanzania inakaribia kuingia katika duru ya Uchaguzi Mkuu Bw. Mohamed Gulam Dewji ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo ambayo ameitumikia kwa muda wa miaka kumi sasa Jimboni mwake. Bw. Dewji ametangaza uamuzi huo jana tarehe 8/7/2015 mjini Singida wakati akiwasomea wananchi wa Jimbo lake taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2005/2010 katika jimbo la Singida Mjini. Akiwahutubia maelfu ya wananchi ambao walikusanyika ili kuisiliza hotuba yake Dewji ameelaza mambo mbalimbali ambayo yamefanikiwa kufanyika katika kipindi chake cha Umbunge jimboni mwake, Dewiji ameeleza kuwa katika kipndi chake chote cha Ubunge  amefanikiwa kusimamia ujenzi wa Shule na kuongeza Vyumba vya Madarasa katika shule mbalimbali Jimboni mwake pamoja na hayo umo pia Ujenzi wa miradi ya Maji ambayo imekwisha kukamilika na kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa jimbo la Singida mjini. Miradi hiyo ni pamoja ule wa Irao na mradi wa maji kutoka Mwankoko ambayo yote kwa pamoja imeingizwa katika mfumo wa maji mkoani Singida (SUWASA), pia vimo visima vya maji ambavyo vinapatikana kwenye mitaa ambayo SUWASA hawajafikisha huduma hiyo ya maji kwa Wananchi.
uchaguzi Mkuu ambao huipatia Tanzania viongozi na wawakilishi wa wananchi katika ngazi mbalimbali ikiwemo ya Urais, Wabunge na Madiwani, aliyekuwa Mbunge wa jimbo wa jimbo la Singida Mjini
   Dewij amesemakuwa hatagombea nafasi hiyo ili kwapisha wengine nao wawatumikie wananchi wa Singida Mjini kwa nafasi hiyo, hata hivyo emeelza kuwa anakabiliwa na majukumu mengine katika biashara za na pia katika Familia yake.

Popular posts from this blog

USIMWACHE MUNGU MAISHANI MWAKO (YESU)

HONGERA FPCT-SINGIDA