Usije ukathubutu kumwacha MUNGU kwa ajili ya kitu chochote, ni heri uache chochote kwa ajili ya MUNGU, Kwa kua katika maisha chochote chaweza kukuacha wakati wowote, Lakini MUNGU hawezi kukuacha, kwa maana atakuwa pamoja nawe siku zote za maisha yako.Furahia uwepo wa MUNGU maishani mwako AMEN.
The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) CHILDREN AND YOUTH MINISTRY (CYM) Jengo la Kanisa la FPCT-SEPUKA IDARA YA WATOTO NA VIJANA FPCT-SINGIDA Idara ya Watoto na vijana ya Misheni ya Singida wamefanya ziara nyingine tena katika kanisa la Fpct-Sepuka ambalo ni moja ya tawi katika Parishi ya Kaselya ambayo imo ndani ya misheni ya Singida na kufanya maombi katika kanisa hilo Pamboja na hayo; pia wamejionea mambo mbalimbali ambayo hayafurahishi katika kanisa hilo kulinganisha na wakati tulionao sasa. Moja ya mambo hayo ni pamoja na uchakavu wa majengo mfano Jengo la kuabudia (kanisa), Nyumba ya Utumishi katika kanisa hilo na maeneo mengine ikiwemo Vyoo n.k. Inasemekana Kanisa lilijengwa zamani kidogo na kufanyiwa ukarabati mdogo mwaka 2000 lakini baada ya hapo limeendelea kuchakaa. Mpaka sasa jengo hilo limebaki kuwa wazi baada ya Milango na madirisha yake kuibwa na ndicho kilicho fanyika hata kwa nyumba ya kanisa hilo ambayo pia haina milango wala madirisha kutokana ...
Wamama wakitoka katika moja ya wodi za wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa Katika kuazimisha siku ya wanawake ulimwenguni Umoja wa Wanawake Watumishi (UWW) wa kanisa la FREE PENTECOSTAL CHURCHES OF TANZANIA-(FPCT) Singida wameazimisha siku yao kwa kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na Mahabusu katika Gereza la Mkoa. Matembezi hayo ya wamama wa Kanisa yaliongozwa na Mwenyekiti wa UWW wa Kanisa hilo Mrs. Betheli (Mama Wawili) ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Watumishi (UWW) kanisa la Free Pentecostal Churches of Tanzania Jimbo la Singida. Pamoja na kufanya matembezi hayo, Wamama hao wamewapatia pole kwa kuwapa vitu mbalimbali kama vile sabuni, mafuta ya kupaka pamoja na mavazi. Pia Mwenyekiti huyo amesifu mapokezi ya wahudumu katika maeneo hayo yote ambayo walifanikiwa kutembelea. Wamama hao wamesema kuwa ni vema kuwakumbuka wenzao wenye shida mbalimbali hasa ...