UWW-SINGIDA KUAZIMISHA SIKU YA MAMA DUNIANI
Wamama wakitoka katika moja ya wodi za wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa |
Katika kuazimisha siku ya wanawake ulimwenguni Umoja wa Wanawake Watumishi (UWW) wa kanisa la FREE PENTECOSTAL CHURCHES OF TANZANIA-(FPCT) Singida wameazimisha siku yao kwa kuwatembelea wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida na Mahabusu katika Gereza la Mkoa. Matembezi hayo ya wamama wa Kanisa yaliongozwa na Mwenyekiti wa UWW wa Kanisa hilo Mrs. Betheli (Mama Wawili) ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Watumishi (UWW) kanisa la Free Pentecostal Churches of Tanzania Jimbo la Singida.
Pamoja na kufanya matembezi hayo, Wamama hao wamewapatia pole kwa kuwapa vitu mbalimbali kama vile sabuni, mafuta ya kupaka pamoja na mavazi. Pia Mwenyekiti huyo amesifu mapokezi ya wahudumu katika maeneo hayo yote ambayo walifanikiwa kutembelea. Wamama hao wamesema kuwa ni vema kuwakumbuka wenzao wenye shida mbalimbali hasa katika siku kama hii.
Wauguzi wakitoa maelezo machache kwa Wamama kabla ya kuingia wodi wa watoto. |
Kwenye picha ni Mrs.Nazael akimpatia mama huyo hongera kwa kujifungua |