Children and Youth Ministry (CYM)
The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT)
CHILDREN AND YOUTH MINISTRY (CYM)
Jengo la Kanisa la FPCT-SEPUKA |
Idara ya Watoto na vijana ya Misheni ya Singida wamefanya ziara nyingine tena katika kanisa la Fpct-Sepuka ambalo ni moja ya tawi katika Parishi ya Kaselya ambayo imo ndani ya misheni ya Singida na kufanya maombi katika kanisa hilo
Pamboja na hayo; pia wamejionea mambo mbalimbali ambayo hayafurahishi katika kanisa hilo kulinganisha na wakati tulionao sasa. Moja ya mambo hayo ni pamoja na uchakavu wa majengo mfano Jengo la kuabudia (kanisa), Nyumba ya Utumishi katika kanisa hilo na maeneo mengine ikiwemo Vyoo n.k. Inasemekana Kanisa lilijengwa zamani kidogo na kufanyiwa ukarabati mdogo mwaka 2000 lakini baada ya hapo limeendelea kuchakaa. Mpaka sasa jengo hilo limebaki kuwa wazi baada ya Milango na madirisha yake kuibwa na ndicho kilicho fanyika hata kwa nyumba ya kanisa hilo ambayo pia haina milango wala madirisha kutokana na kuibwa na watu wasiojulikana
.
Ombi letu kama vijana, tunawaomba Viongozi wa misheni yetu ya Singida kuliangalia kwa jicho lingine kanisa hilo ili kulifanya liwe thabiti katika kuihubiri Injili ya Kristo kwa kuyatengeneza na kuyaboresha Mazingira ya Kanisa hilo.Ziara nyingine ya vijana hao wa Fpct Misheni ya Singida inatarajiwa kufanyika katika Parishi ya Unyianga ambako kutakuwa na mengi huko pia yatafanyika