Posts

Showing posts from January, 2017

Children and Youth Ministry (CYM)

Image
The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) CHILDREN AND YOUTH MINISTRY (CYM) Jengo la Kanisa la FPCT-SEPUKA IDARA YA WATOTO NA VIJANA FPCT-SINGIDA Idara ya Watoto na vijana ya Misheni ya Singida wamefanya ziara nyingine tena katika kanisa la Fpct-Sepuka ambalo ni moja ya tawi katika Parishi ya Kaselya ambayo imo ndani ya misheni ya Singida na kufanya maombi katika kanisa hilo Pamboja na hayo; pia wamejionea mambo mbalimbali ambayo hayafurahishi katika kanisa hilo kulinganisha na wakati tulionao sasa. Moja ya mambo hayo ni pamoja na uchakavu wa majengo mfano Jengo la kuabudia (kanisa), Nyumba ya Utumishi katika kanisa hilo na maeneo mengine ikiwemo Vyoo n.k. Inasemekana Kanisa lilijengwa zamani kidogo na kufanyiwa ukarabati mdogo mwaka 2000 lakini baada ya hapo limeendelea kuchakaa. Mpaka sasa jengo hilo limebaki kuwa wazi baada ya Milango na madirisha yake kuibwa na ndicho kilicho fanyika hata kwa nyumba ya kanisa hilo ambayo pia haina milango wala madirisha kutokana ...